1 min read
08 Nov
08Nov

Gharama kubwa za tiketi kwa usafiri wa anga imekua moja ya kikwazo kikubwa kinachokwamisha sekta ya utalii barani Afrika.

Haya yamezungumzwa katika mkutano kuhusu utalii yaani WORLD TRAVEL AND TOURISM COUNCIL (WTTC) uliofanyika jijini Kigali nchini Rwanda.

Wadau kutoka nchi mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wamesema "Kuna gharama ndogo kusafiri kutoka Afrika kwenda Bara lingine kuliko kusafiri ndani ya Africa. Nauli ya ndege kutoka Berlin Germany kwenda Istanbul Uturuki inagharimu dola 150 na safari huchukua chini ya masaa matatu, lakini cha kushangaza, nauli ya ndege kutoka Kinshasa Congo kwenda Lagos Nigeria hugharimu Dola 500 na safari huchukua hadi masaa 20.

Swala hili la kuwepo kwa kodi kubwa na nauli kubwa hufanya shughuli nzima za kitalii kuwa ngumu na kuzifanya nchi zetu za Afrika kukosa mapato.

Comments
* The email will not be published on the website.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING