Mwanafunzi wa miaka 13 wa shule ya msingi nchini Serbia anashikiliwa na polisi kwa kosa la kuua wanafunzi wenzake 8 darasani.
Tukio hilo limesababisha baba na mama wa mtoto huyo kukamatwa kwa mahojiano. Imeripotiwa kuwa mtoto huyo alichukua bunduki ya baba yake ambae anamiliki silaha hiyo kwa uhalali na kwenda shuleni kufanya shambulio hilo darasani na kujeruhi wenzake nane (8) akiwemo mwalimu mmoja na mlinzi wa shule hiyo.
Hadi kufikia leo chanzo na malengo ya shambulio hilo liolilofanywa na kijana mdogo hakijajulikana ni nini. Kijana huyo amepelekwa kliniki kwa ajili ya utafiti na uchunguzi zaidi.
Kulingana na Sheria ya nchi ya Serbia kijana huyo hatoweza kuhukumiwa kwa kuwa yupo chini ya umri.