Wananchi nchini Nigeria wametoa malamiko kwa serikali mara baada ya serikali ya nchi hiyo kutangaza kuwa Rais Muhamaddu Buhari atabaki nchini Uingereza kwa wiki moja zaidi kwa ajili ya matibabu ya meno.
Taarifa hiyo ilizua malalamiko kwa raia wengi ambao wamedai Rais hajashughulikia masuala muhimu yanayoikabili nchi ikiwemo usalama na hali duni ya maisha.
Rais Muhammadu Buhari alisafiri kwenda nchini Uingereza kwa ajili ya kuhudhuria kutawazwa kwa mfalme wa Uingereza Charles III.