1 min read
09 Jun
09Jun

Inawezekana kuonekana ni tukio la kushangaza zaidi kuwahi kutokea tanzania na hata duniani kwa ujumla.

Mama mmoja anayetambulika kwa jina la Jamila wilayani Bagamoyo amejifungua mtoto mwenye upungufu wa viungo ikiwemo kichwa.

Daktari wa hospitali hiyo ya wilaya ya Bagamoyo ndugu, Gasper Mbaga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akibainisha kuwa mama huyo alikua akihudhuria hospitali kwa ajili ya huduma ya kliniki na alikua akiendelea vizuri kwani mtoto aliyekua tumboni alikua hai na akicheza kama ilivyo kawaida.

Aidha mtoto huyo alizaliwa na mapungufu mengine kama kuwa na miguu iliyopinda huku jinsia yake ikiwa haieleweki vizuri kama ni ya kike au ya kiume.

Mtoto huyo alifariki mda mchache baada ya kuzaliwa.

Comments
* The email will not be published on the website.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING