1 min read
14 Aug
14Aug

Nimekuwa nikipokea jumbe nyingi za whatsp pamoja na emails kutoka kwa watu tofauti wakitaka niandike article kuhusu namna gani mwanaume anaweza kugundua mwanamke sahihi wa kuanzisha nae maisha na hatimaye kufunga nae ndoa. Leo ninakuletea article hii ambayo inaelezea dalili au mbinu unazoweza kutumia kujua kama mpenzi wako ni Wife material au ni Girlfriend material. Karibu!!! 


 - Girlfriend material ni MTUMIAJI (A BIG SPENDER)

Girlfriend material ni yule msichana ambaye ukiwa nae matumizi yako ya fedha yanaongezeka na kuwa makubwa sana kupita kipato chako. Madada wa aina hii wana gharama kubwa kupita hata kodi za serikali. Unapotoka nae out labda kwenye restaurant hukimbilia kuagiza vyakula au kitu chenye thamani kubwa bila ya kujali uwezo wako wa kifedha. Ukifanya masihara unaweza ukakuta amekuja na kikosi cha marafiki zake.

Wife material huonea huruma fedha yako (WIFE MATERIAL IS CONSERVATE)

Unapo-date na wife material, jaribu kumpeleka kwenye restaurant au duka, ni lazima atauliza gharama ya hicho chakula au bidhaa kabla hajaagiza. Wakati mwingine huweza kukataa hata kile unachomwagizia kwa sababu ya ukubwa wa gharama. Wife material anajua thamani ya pesa zako na hayuko tayari kuona unatumia pesa nyingi.

couples at restaurant

Girlfriend material ni wa kila mtu (GIRLFRIEND MATERIAL IS FOR EVERYBODY)

Girlfriend ambaye kila saa anapokea simu utadhani ni customer care agent au kuchat wakati mwingi unapokua naye ni dalili mbaya kuwa huyo siyo mwanamke wa kutengeneza nae future. Girlfriend ambaye mara anaonekana na mwanaume huyu mara yule, mara ameshushwa na gari nyeupe, kesho gari nyeusi, ambaye kila mara anakuomba pesa au zawadi bila kujali uwezo wako, ukiwa nae mara katoa mlio wa kwenye simu, mara simu kaiweka kwa kuifunika usione anayempigia au kum-text huyu siyo mwanamke kuwa makini nae sana. 

Wife material ni wa ‘mtu mmoja’ (WIFE MATERIAL BELONGS TO ONE MAN) 

Mwanamke ambaye ni wife material hawezi kuwa ni mtu wa kila mtu. Mwanamke wa aina hii huwa na heshima kwa mpenzi wake na huwa anafanya kila linalowezekana kulinda heshima yake na mwanaume wake. Huwezi kumuona akiwa busy kupoteza muda wake katika mambo ambayo hayana umuhimu kwake. Hawa siyo wanawake wa kila kukicha kudai pesa ya sare ya shughuli. Kwa leo naomba niishie hapa, nitaendelea kuandaa article zingine zinazoelezea njia za kukuwezesha kujua kama wewe una-date na wife material au girlfriend material. Kama umependa article hii tafadhali usisite kuacha comment yako. Asante!!

Comments
* The email will not be published on the website.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING