1 min read
06 Jan
06Jan

Raia nchini Afrika kusini wamepokea kwa maoni tofauti kuhusiana na kuachiwa huru kwa aliyekua nyota wa riadha wa mashindano ya Olympic Oscar Pistorius ambaye wengi walimfahamu kwa uhodari wake wa kukimbia riadha huku akiwa mlemavu akitumia miguu maalum ya bandia. Oscar Pistorious alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela kwa kosa la kuua  kwa kumpiga risasi aliyekua mpenzi wake Bi, Reeva Stenkamp mwaka 2013. 

Oscar alipatiwa msamaha wa kutoka jela baada ya kutumikia kifungo kwa miaka Tisa (9) huku akiwa amebakisha Minne (4). Mahakama iliamua kumuachia huru huku akitakiwa kuishi kwa uangalizi maalum akiwa uraiani. 

Maoni yamekua tofauti baada ya Oscar kuachiwa huru, baadhi ya watu walitoa maoni wakisema mahakama imefanya jambo jema na ni haki kuona mtu anapatiwa msamaha kwa makosa aliyoyafanya ikiwa ameonyesha moyo wa utiifu gerezani.

Comments
* The email will not be published on the website.
I BUILT MY SITE FOR FREE USING